Header Ads

𝐈𝐓𝐈𝐆𝐈 𝐘𝐀𝐉𝐈𝐕𝐔𝐍𝐈𝐀 𝐌𝐀𝐅𝐀𝐍𝐈𝐊𝐈𝐎 𝐌𝐀𝐊𝐔𝐁𝐖𝐀 𝐓𝐀𝐍𝐆𝐔 𝐈𝐀𝐍𝐙𝐄 𝐊𝐔𝐒𝐇𝐈𝐑𝐈𝐊𝐈 𝐍𝐀𝐍𝐄𝐍𝐀𝐍𝐄 𝐊𝐈𝐓𝐀𝐈𝐅𝐀

Afisa Biashara wa Halmahauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida, Richard Mmuni katika  Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa 2026 yanayo endelea Uwanja wa Maonesho wa Dk. John Samuel Malecela Jijini Dodoma Agosti 7, 2026.

........................

HALMASHAAURI ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida inajivunia mafanikio makubwa tangu ianze kushiriki Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa sasa ikiwa ni miaka 9 inashiriki.

Hayo yameelezwa na Afisa Biashara wa Halmahauri hiyo, Richard Mmuni katika  Maonesho ya Wakulima Nanenane Kitaifa 2026 yanayo endelea Uwanja wa Maonesho wa Dk. John Samuel Malecela Jijini Dodoma Agosti 7, 2026.

“Ushiriki wa Halmashauri yetu katika maonesho haya kumekuwa na tija kubwa hasa kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana kwenye sekta mbalimbali,” alisema Mmuni. 

Awali ya yote Mmuni ameipongeza Serikali chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fursa ya kuandaa Maonesho hayo ambayo ni ya muhimu kwa taifa hasa wakati huu ambao sekta ya kilimo inapewa nafasi kubwa katika kuchangia pato la taifa.

Mmuni alisema katika Halmashauri ya Wilaya ya Itigi ina fursa mbalimbali inayoshughulika nazo ikiwemo sekta ya kilimo.

“ Halmashauri yetu ni kinara kwa kilimo cha dengu kwa msimu uliopita tulifanikiwa kuuza tani 17,207 na baada ya kuziuza tulipata jumla ya Shilingi bilioni 19 ambazo zilienda kwa wakulima na kuinua uchumi wao kutoka wa chini kwenda juu,” alisema Mmuni. 

Mmuni alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wawekezaji, wakulima na wafanyabiashara  kwenda katika wilaya hiyo kuwekeza kwani bado wana maeneo ya kutosha kwa kilimo cha dengu ambalo ni zao zuri na linaongeza thamani na uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Mmuni alisema kuwa pia halmashauri hiyo kutokana na kuwa na misitu mikubwa pia inajishughulisha na ufugaji wa nyuki na kupatikana kwa mazao yake kama asali yenye ubora wa juu.

Aliongeza kusema kuwa katika halmashauri hiyo inavikundi 11 vya ujasiriamali ambavyo vinajishughulisha na  mazao yanayotokana na nyuki.

Alisema wana mizinga 42 ya kisasa  na mizinga 85 ya kienyeji ambayo imesambazwa katika misitu mbalimbali iliyopo kwenye halmashauri hiyo.

“Katika Maonesho haya ya wakulima hapa Dodoma tumekuja na asali yetu nzuri hivyo tunawakarisha wananchi na wadau mbalimbali kufika kwenye banda letu kuona na kununua bidhaa mbalimbaali zinazotokana na nyuki,” alisema Mmuni. 

Aidha, Mmuni alisema kuwa katika halmashauri yao inajishughulisha na ufugaji wa ng’ombe, mbuzi na kuku.

Alisema katika eneo la kilimo pia wanalima zao la alizeti ambalo linatoa mafuta yanayofaa kwa afya ya binadamu na mashudu ambapo anawahamasisha wawekezaji kwenda kulima zao hilo.

Katika Maonesho hayo wamefika na bidhaa mbalimbali zinazotokana na shughuli wanazozifanya katika Halmahauri ya Wilaya ya Itigi, kama unga waa dengu, mafuta ya alizeti na zile zinazotokana na nyuki hivyo anawakaribisha wananchi kufika katika banda lao kujipatia kwa bei nzuri kabisa.Mmoja wa Wananchi akihudumiwa alipotembelea Banda la Halmashauri ya Wilaya ya Itigi katika Maonesho hayo.

Habari hii imeandaliwa na Dotto Mwaibale namba ya simu 0754362990.

No comments

Powered by Blogger.