COSTECH INAVYO SAIDIA WABUNIFU NCHINI
COSTECH
imekuwa ikitoa ushauri na Rasilimali fedha kwa wabunifu mbalimbali.
Miongoni mwa
wabunifu hao ni Dk. Cecilia Rolence China ambaye ni mwanasayansi mahiri Mwanamke na Mhadhiri.
China amepata
umaarufu mkubwa kitaifa na kimataifa kutokana na ugunduzi wake wa kimapinduzi
wa kutumia maganda ya korosho na kutengeneza dawa asili na rafiki wa mazingira ambayo
inatumika kutengeneza ngozi.
Dk.China akizungumza
kwenye Maonesho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayoendelea
kwenye viwanja vya Usagara Jijini Tanga amesema kuna wadau mbalimbali wa
kimataifa na kitaifa waliomwezesha kufikia hatua hiyo yenye mafanikio makubwa.
Ameyataja
baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni kuanzisha Kampuni ya AfriTech Organic Leather.
Alisema kampuni
hiyo inazalisha ngozi ghafi zilizosindikwa kwa maganda ya korosho na
kutengeneza bidhaa za ziada kama mikoba ya kike, pochi, na vifaa vya ofisini
vyenye ubora wa kimataifa.
“ Kampuni yangu ya kipekee ya kiteknolojia ya kuchakata takataka za korosho na kuzigeuza kuwa kemikali salama ya ngozi imesajiliwa kisheria na kupata hataza ya kiugunduzi na kunipa umiliki wa teknolojia duniani,” alisema China.
Alisema kupitia
taasisi yake, amefanikiwa kutoa mafunzo ya vitendo (Capacity Building) kwa
zaidi ya wanawake na vijana 300.
Mafanikio
mengine yaliyopatikana ni kujifunza mnyororo mzima wa thamani wa ngozi (kuanzia
usindikaji wa asili hadi ushonaji wa bidhaa.
Aliongeza
kuwa COSTECH kupitia mfuko wa Serikali wa kusaidia wabunifu imekuwa ikitoa ruzuku ndogo ndogo na gharama za kuwezesha ushiriki wake kwenye
maonesho ya kitaifa ya ugunduzi, jambo lililomsaidia kupata mtaji wa awali wa
majaribio ya kijamii.
Alitaja
baadhi ya taasisi na wadau wengine waliomsaidia rasilimali fedha ulitokana na ruzuku za kiutafiti na ufadhili wa masomo ya
juu kutoka mashirika makubwa ya kimataifa na kikanda.chini ya UNESCO.
Alisema
UNESCO ndiyo taasisi iliyompa msukumo
mkubwa zaidi wa kifedha ambapo iliweza kumtunuku ruzuku ya Tuzo ya Fellowship
ya takriban USD 50,000 (zaidi ya Shilingi Milioni 130 za Kitanzania).
“Fedha hizi zilitumika kununulia vifaa vya kisasa vya kimaabara, kemikali za majaribio, na kuajiri wasaidizi wa utafiti ili kuongeza kasi ya uzalishaji wa dawa hiyo ya maganda ya korosho.
Taasisi
nyingine ni Benki ya Maendeleo ya Afrika, ambayo ilifadhili masomo yake ya
ngazi ya juu ya Uzamivu (PhD).
Aliongeza kuwa ufadhili huo uliondoa vikwazo vya
kifedha na kumruhusu kujikita kikamilifu katika utafiti uliomfikisha kwenye
ugunduzi huo wa kipekee.
Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dk. Amos Nungu, akizungumza kwenye Maonesho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu yanayofanyika katika viwanja hivyo jijini humo akieleza maendeleo ya tafiti na bunifu zinazofanyika nchini alisema Tanzania ina ubunifu wa aina mbalimbali, ikiwemo unaolenga kuongeza thamani katika mazao ya kilimo, mifugo na maeneo mengine mbalimbali.
“Kwa upande wa tafiti tuko vizuri kama nchi, tunatoa nafasi ya kuboresha,” alisema Dk. Nungu.
Alisema
kuwa,baadhi ya wabunifu wamekuwa wakifanya mambo yenye kuleta athari chanya
katika jamii kupitia tafiti na bunifu zao.
Mbunifu mwingine aliyewezeshwa na COSTECH Lusano Luvanda ambaye ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), na Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa kampuni au maabara ya ubunifu ya Ecoflame Labs na Beyond Horizon, inayojihusisha na masuala ya teknolojia na ujasiriamali wa vijana mbunifu wa kifaa kinachoitwa Atlas kinachotengeneza nishati gas ya kupikia kutoka kwenye maji akizungumzia ubunifu wake.
Alisema
alisukumwa na dhamira ya kutengeneza nishati ya umeme kwa ajili ya matumizi ya
nyumbani.
Aidha, Luvanda
alisema baada ya ubunifu huo alisaidiwa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Te
knojia
cha Mbeya (MUST) ambapo amewaomba wawekezaji kusaidia ubunifu huo ili kuifanya
nchi yetu kuacha matumizi ya kutumia nishati kama petroli kutoka nje ambayo
inapatikana kwa gharama kubwa na kuchangia uharibifu wa mazingira.
“Naishukuru
COSTECH kwa kuniwezeha kufikia hatua kubwa ya ubunifu wangu kwa kunipa fedha
tangu nilipoanza ubunifuu ambao umeonesha tija,” alisema Luvanda.
Wabunifu
wengine ambao wameishukuru COSTECH ni Maganga Mabula ambaye amebuni mfumo
unaoitwa Mnyama Check App na Heleni Janja.
Mfumo huo
unasaidia wakulima kujua afya za wanyama wanaofuga na mahali walipo.
Mbunifu mwingine kutoka COSTECH, Ibrahim Meshack ambaye amebuni mashine ya kukokotwa ijulikayo kama Smart Shamba Planter mahususi kwa upandaji wa mbegu mbalimbali kama, mahindi, mpunga. Dengu, karanga na mazao mbalimbali.
Meshack alitaja sifa ya Planter hiyo ni kupanda kwa muda mfupi na kwa gharama nafuu na inaweza kuvutwa kwa guta, Power Tiller na trekta.
“Planter hii inakwenda kuongeza wingi wa mazao shambani na kipato,” alisema Meshack.
Dk. Cecilia China akionesha vifungashio vyenye kemikali zilizotengenezwa na kampuni yake kwa ajili ya kutengeneza ngozi.
Mbunifu kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Ibrahimu Meshack akitoa maelezo ya Planter aliyoibuni kwa ajili ya kupanda mbegu mbalinbali.
Bidhaa za ngozi zinazotengenezwa na Kampuni ya AfriTech Organic Leather inayo milikiwa na Dk. Cecilia China.Kemikali za kutengeneza ngozi zinazotengenezwa na Kampuni ya AfriTech Organic Leather inayo milikiwa na Dk. Cecilia China.



No comments