Header Ads

NDG. ABDI AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA WA VIUNGO KIZIMBANI

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, ameahidi kushirikiana na taasisi husika kutatua changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wa bidhaa za viungo (Spice) katika eneo la Kizimbani, Zanzibar.

Ndugu Abdi ametoa ahadi hiyo baada ya kuwatembelea wafanyabiashara hao katika eneo lao la biashara, ambapo amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kuendesha shughuli zao na kujikwamua kiuchumi.

Amesema changamoto zilizowasilishwa na wafanyabiashara hao zitafanyiwa kazi kwa kushirikiana na taasisi zinazohusika, ili kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati na kuwawezesha kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.

Kwa upande wao, wafanyabiashara hao wamemuomba Ndugu Abdi kuwasaidia katika kutatua changamoto ya upatikanaji wa mikopo, ambayo itawawezesha kuongeza mitaji, kupanua biashara zao na kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Wamesema upatikanaji wa mitaji ya kutosha utawasaidia kuongeza uzalishaji na kukuza biashara ya bidhaa za viungo, ambayo ni miongoni mwa shughuli zinazowapatia kipato na kuchangia katika uchumi wa Zanzibar.

No comments

Powered by Blogger.