PROFESA MSOFFE: WANANCHI TUNZENI CHAKULA KUELEKEA MVUA ZA VULI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Pro. Peter Msoffe, akizungumza na wananchi kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Chakula Duniani alipotembelea na kukagua mabanda ya maonesho katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara jijini Tanga.
.........................
Na Hamida Kamchalla, Tanga
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Pro. Peter Msoffe amewataka wananchi kutunza chakula hasa kipindi hiki kuelekea mvua za vuli zitakazo ambatana na elnino zinzotabiriwa kunyesha nchini hivi karibuni.
Wito huo ameutoa leo kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kitaifa ya Chakula Duniani alipotembelea na kukagua mabanda ya maonesho katika viwanja vya shule ya sekondari Usagara jijini Tanga.
Prof. Msoffe amesema kuwa kulingana na utabiri wa hali ya hewa uliotolewa na TMA, Mkoa wa Tanga ni miongoni mwa Mikoa itakayopata mvua ya elnino hivyo inapaswa wananchi kujiandaa kwa kutunza chakula na miundombinu inayohusika na mifumo ya chakula nchini kuanzia uzalishaji hadi uhifadhi.
"Utunzaji wa chakula ni suala la kiibada, mvua hizi zinaweza kuleta madhara mistype chakula, mkiwa majumbani au kwenye sherehe kumbukeni kutunza chakula, wewe unatupa jalalani mwengine anakutafuta" amesema.
Aidha amefafanua kwamba amefarijika sana kuona bunifu mbalimbali zilizofanyika katika mabandanda jinsi wajasiriamali walivyoongeza thamani ya bidhaa za kilimo, kuanzia nafaka, mikunde kunde, mboga za majani na matunda amesema.
"Lakini pia nimefurahishwana wafanyabiashara mbalimbali wanaouza vifaa vya kilimo, vingine vinahusiana na umwagiliaji, hii yote inaonesha kwamba muitikio huu ni kuunga mkono juhudi za serikali.
Pia amebainisha serikali ya sasa imejipambanua wazi kwamba imedhamiria kufanya mageuzi katika sekta ya kilimo kwa lengo likiwa ni kuhakikisha usalama wa chakula, lakini pia kilimo kunakuwa sio cha mazoea.
Utembeleaji mabaanda ukiendeleaMaonesho yakiendelea.





No comments