Header Ads

TAARIFA KWA UMMA URASIMISHAJI WA MATUMIZI YA MBEGU ZA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA (TARI)

Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dk. Thomas Bwana

.................. 

Dodoma, Oktoba 09,2026.

TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inapenda kuwataarifu wadau wote wanaojihusisha na uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mbegu zinazomilikiwa na Taasisi kuwa ni wajibu wao kuhakikisha wanazingatia taratibu za haki miliki, ikiwemo kusaini mikataba rasmi ya matumizi (Licensing Agreements) na kulipa mirabaha stahiki kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 30 vikisomwa pamoja na Kifungu cha 40 cha Sheria ya Haki Miliki za Ugunduzi wa Mbegu za Mimea (Plant Breeders' Rights Act), pamoja na Kanuni ya 33(b) ya Kanuni za Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania, 2023, TSN. 448 la tarehe 30 Juni 2023.

Kwa mantiki hiyo, TARI inatoa wito kwa wazalishaji, wasambazaji, wauzaji, kampuni, taasisi na mtu yeyote anayejihusisha au anayetarajia kuanza kuzalisha, kusambaza au kuuza mbegu au teknolojia nyingine yoyote inayomilikiwa na TARI, kuwasiliana na Taasisi ndani ya kipindi cha siku thelathini (30) na kipindi hicho cha siku 30  kikiisha, TARI itachukua hatua za kisheria dhidi ya wadau wote watakaoshindwa kutekeleza wito huu.

Lengo la tangazo hili ni kuwataka wadau: i. Kujisajili ii. Kuhakiki na kuhuisha taarifa zao iii. Kusaini mikataba rasmi ya matumizi ya teknolojia na mbegu za TARI; na iv.

 Kuweka utaratibu sahihi wa ulipaji wa mirabaha kwa mujibu wa Sheria na Kanuni. Taarifa hili imetangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali Namba.18012 la tarehe 9 Oktoba, 2026. 

Taarifa ziwasilishwe kwa anuani ifuatayo: Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), S.L.P. 1571, Dodoma, Tanzania. Barua pepe:

dg@tari.go.tz  Mawasiliano: 0733543194 “TARI-UTAFITI KWA MAENDELEO YA KILIMO” TAARIFA KWA UMMA URASIMISHAJI WA MATUMIZI YA MBEGU ZA TAASISI YA UTAFITI WA KILIMO TANZANIA (TARI) Dodoma, Oktoba 09,2026.

 Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inapenda kuwataarifu wadau wote wanaojihusisha na uzalishaji, usambazaji na uuzaji wa mbegu zinazomilikiwa na Taasisi kuwa ni wajibu wao kuhakikisha wanazingatia taratibu za haki miliki, ikiwemo kusaini mikataba rasmi ya matumizi (Licensing Agreements) na kulipa mirabaha stahiki kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 30 vikisomwa pamoja na Kifungu cha 40 cha Sheria ya Haki Miliki za Ugunduzi wa Mbegu za Mimea (Plant Breeders' Rights Act), pamoja na Kanuni ya 33(b) ya Kanuni za Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania, 2023, TSN. 448 la tarehe 30 Juni 2023.

Kwa mantiki hiyo, TARI inatoa wito kwa wazalishaji, wasambazaji, wauzaji, kampuni, taasisi na mtu yeyote anayejihusisha au anayetarajia kuanza kuzalisha, kusambaza au kuuza mbegu au teknolojia nyingine yoyote inayomilikiwa na TARI, kuwasiliana na Taasisi ndani ya kipindi cha siku thelathini (30) na kipindi hicho cha siku 30  kikiisha, TARI itachukua hatua za kisheria dhidi ya wadau wote watakaoshindwa kutekeleza wito huu. Lengo la tangazo hili ni kuwataka wadau: i. Kujisajili ii.

 Kuhakiki na kuhuisha taarifa zao iii. Kusaini mikataba rasmi ya matumizi ya teknolojia na mbegu za TARI; na iv. Kuweka utaratibu sahihi wa ulipaji wa mirabaha kwa mujibu wa Sheria na Kanuni. Taarifa hili imetangazwa rasmi kwenye Gazeti la Serikali Namba.18012 la tarehe 9 Oktoba, 2026.  Taarifa ziwasilishwe kwa anuani ifuatayo: Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), S.L.P. 1571, Dodoma, Tanzania. Barua pepe: dg@tari.go.tz  Mawasiliano: 0733543194 “TARI-UTAFITI KWA MAENDELEO YA KILIMO”

No comments

Powered by Blogger.