KIJUE KILIMO BORA CHA MIWA
Kilimo cha miwa ni kilimo chenye tija kwa mkulima,
kilimo hiki kinaweza kufanywa na mtu yeyote yule aidha awe ameajiliwa au laaa.
Kuna aina kuu 2 za miwa:
1. BUNGALA
2. MIWA MYEKUNDU
Unachotakiwa kufanya katika kulima kilimo hiki ni, Kwanza kabisa tafuta
aridhi.
Tafuta mbegu ya miwa ya BUNGALA miwa hii ni laini sana na ni rahisi
kuichana kwa kutumia meno, baada ya kupata miwa hii kata vipande vipande vya
pingili tatu.
Kumbuka kwamba miwa ni rahisi sana kushambuliwa na mchwa, Ili kuzuia
isiliwe na mchwa nenda katika maduka ya kilimo na ununue viuatilifu au
wasiliana nasi @kilimo_tz
FURSA
Soko la muwa ni kubwa sana, maana viwanda vingi vya sukari hapa Tanzania
vinahitaji miwa, na mashamba ya miwa yaliopo hayatoshelezi mahitaji.
Hivyo viwanda hivi vya sukari viko tayari kununua miwa kutoka kwa wakulima
ili kupata mahitaji ya maligafi ambayo ni miwa.
UPANDAJI WA MIWA
Hakikisha unapokuwa unapande miwa yako acha nafasi ya mita moja (1m) kati
ya mche na mche, pia mita moja (1m) kati ya mstari na mstari.
Unapokuwa unapanda miwa hii hakikisha hizo pingili zote 3 zimezama ndani ya
ardhi na kipande kidogo tu ndio kibakie juu ya uso wa ardhi, katika wa nyuzi
30.
Kwenye ploti ndogo ya mita 50 kwa mita 70, utakuwa na miche 70×50=3500
(mashina elfu tatu na mia tano).
SHARE NA NDUGU ZETU WENGINE ILI TULEGEZE VYUMA
INUKA Tanzania INUKA Afrika Mashariki- Ufugaji na Kilimo cha Kisasa
INAENDELEA.....
#kilimochamiwa #miwa #kilimochamiwa #mashambayamiwa #sokolamiwa #sukari
#viwandavyasukari #sugarcane #sugarcanefarming #mbeguzamiwa
#dripirrigationsystem #kilimochamatone #kilimochaumwagiliaji #kilimochakisasa
Simu:
+255 712 25 31 02(WhatsApp)
+255 692 43 02 63
Email:
kilimotz3@gmail.com


No comments