Header Ads

RAIS DKT. SAMIA AWATAKA WAKULIMA KULIMA KARAFUU KWA WINGI NA KWA TIJA ZAIDI


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka wakulima wa karafuu kuacha kuchepusha na kuuza kwa magendo zao la karafuu.

Rais Samia ameyasema hayo leo mara baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi la Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC), Madungu Chake Chake Pemba.

Aidha, Rais Samia amewataka wakulima kuendelea kulima karafuu kwa wingi na kwa tija zaidi ili kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo na kuinua uchumi wa buluu.

Vile vile, Rais Samia amesema serikali itaendelea kutafuta fursa za kuongeza tija na uzalishaji bila ya kuathiri viwango na thamani ya karafuu ya Zanzibar katika soko la kimataifa.

Kwa upande mwengine, Rais Samia ametoa wito kwa ZSTC kutatua kero za wakulima wa karafuu pamoja na kuwa na kanzidata ili kutunza kumbukumbu za zao hilo na wakulima zitakazowezesha kuratibu mipango endelevu.

Halikadhalika, Rais Samia amewataka ZSTC kutumia ipasavyo jengo lililozinduliwa ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ikiwemo kukusanya mapato yatakayolisaidia Shirika kujiendesha lenyewe na kupunguza utegemezi kwa serikali.

No comments

Powered by Blogger.