Header Ads

KILIMO BORA CHA ZAO LA SOYA

Muonekano wa zao la Soya
 Utangulizi: 

..............................

Na Mwandishi Wetu

Soya (Glycine  max) ni  zao  la  jamii  ya  mikunde  ambalo  asili  yake  ni    ni  Bara  la  Asia  katika nchi   ya   China   ambako lilianza   kulimwa  takribani   miaka   4800   iliyopita.   Zao   hili   

lilililiingizwa    hapa    nchini    katika    mnamo mwaka    1907    katika    maeneo    ya    Amani    wilayani   Muheza   katika   mkoa   wa   Tanga.   

Kilimo   cha   zao   hili   kiliendelea   kupanuka katika  miaka  ya  1930  na  1960  na  kuenea  katika   mkoa   wa   Mtwara,   Morogoro,   na  Ruvuma.  Kutokana  na  uhamasishaji  juu  ya  

matumizi ya soya kwa lishe.  

Kwa  sasa  mikoa  inayoongoza  kwa  uzalishaji  

ni  pamoja  na  Ruvuma,  Mbeya,  Rukwa,  Iringa  na  Morogoro.  Mikoa  mingine  inayofaa  kwa kilimo cha zao hili ni pamoja na Tanga, Lindi, Kagera,  Mara,  Kigoma,  Kilimanjaro,  Arusha  na Manyara.

AINA ZA SOYA: 

Zipo  aina  mbalimbali  za  soya,  hapa  nchini aina zinazozalishwa ni pamoja na 

1. Bossier, 

2. Uyole soya  1,  

3. Ezumu  Tumu,  

4. Delma  Hermon,  

5. Duiker  na  

6. Kaleya.

Aina  hizi  hutofautiana  katika  kustawi na  kutoa  mavuno  hata  hivyo  soya  aina  ya  Bossier huweza  kustawi  katika  maeneo  mengi  zaidi hapa nchini.

MAZINGIRA YANAYOFAA KWA UZALISHAJI:

Soya  huhitaji  mvua  ya  kutosha  ya  wastani  wa  milimita    350    hadi    1,500    kwa    mwaka inayonyesha   katika   mtawanyiko   mzuri   au  umwagiliaji maji ili kuhakikisha upatikanaji wa 

unyevu  wa  kutosha  kuanzia  upandaji  hadi  inapotoa   maua   na   matunda.   Uvunaji   ni   muhimu   ufanyike   wakati   hakuna   mvua   ili kuruhusu   soya   kukauka   vizuri na kutunza ubora wake. 

Soya  kama  yalivyo  mazao  mengine,  huhitaji udongo  wenye  rutuba  na  usiotuamisha  maji. Hivyo kama shamba halina rutuba ya kutosha, ni   muhimu   kutumia   mbolea.   Mbolea   za   

viwandani  zinazoweza  kutumika  ni  aina  ya DAP na TSP (wastani  wa  kilo  80  hadi  100 kwa  hekta  moja)  kwa  ajili  ya  kupandia  na (wastani  wa  kilo  60  hadi  80  kwa  hekta)  za  

mbolea  ya  kukuzia  kama  CAN.  Ni  muhimu kupata  ushauri  wa  kitaalam  juu  ya  rutuba  ya udongo kabla ya kuamua kutumia mbolea.  

UZALISHAJI: 

Ni  muhimu  kuzingatia  misimu ya mvua ya mahali  husika  na  aina  ya  soya  inayofaa ili kuruhusu  soya  kukomaa  wakati  hakuna  mvua na hivyo kuhifadhi ubora wake.  

1.  Shamba  liandaliwe  kwa  kuondoa  magugu na  kutifuliwa. Soya  inaweza  kupandwa  katika matuta au katika mistari. 

2.  Nafasi  inayofaa  katika  kupanda  soya  ni Sm.5  hadi  10  kati  ya  mashina  na  Sm. 45  hadi 60 kati ya mstari na mstari kutegemea aina ya soya na rutuba ya udongo.  

3.  Kila  shimo  lipandwe  mbegu  moja  katika kina  cha  sentimita  2  hadi  tano  na  kufukiwa vizuri kwa udongo. 

4. Palizi ifanyike kuondoa magugu, ikiwa soya itastawi na kufunika  udongo vizuri inaweza kupunguza uhitaji wa kupalilia zaidi. 

5. Soya  huchukua  wastani  wa  miezi  mitatu hadi   saba kukomaa   kutegemea   na   aina, mahali ilikopandwa na utunzaji wa shamba. Ni  vema  kuvuna  soya  mara  inapokomaa  na  kuanza kukauka. 

6.  Soya  iliyovunwa  itolewe  maganda  na kukaushwa vizuri  tayari  matumizi  au.kwa kuhifadhi. 

7. Mavuno  yanaweza  kuwa  kilo 2000 hadi 3,500  kwa  hekta    sawa  na  kilo 800 hadi 1,400 kwa ekari moja kutegemea na aina na 

mazingira ya uzalishaji.

MAGONJWA NA MADUDU:

Zao la soya halishambuliwi sana na magonjwa na wadudu. Inafaa   kuzingatia   kanuni za kilimo  bora    na  kupata  ushauri  wa  kitaalamu hasa inapolazimu kutumia madawa ya wadudu na   magonjwa.  Ni muhimu kuzingatia matumizi ya mbegu safi (zisizo na vimelea vya magonjwa)  na  kutumia  mbinu  za  mzunguko  

wa mazao. 

MAANDALIZI YA SOYA: 

Ni  muhimu  kuondoa  kemikali  zisizofaa  kabla  

ya  kutumia  soya  kwa  lishe.  Zingatia  hatua  

zifuatazo:- 

1.Chemsha maji 

2.Tumbukiza soya kidogo kidogo ili iendeleekuchemka  

3.Baada ya kuweka soya  kwenye maji yanayochemka, chemsha  kwa  dakika 30 ili kuondoa kemikali zisizofaa. 

4. Opoa, suuza na maji safi. 

5. Anika hadi zikauke 

6. Saga kupata  unga kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Unga  wa  soya unaweza kutumika  katika upishi  wa  vyakula  kama  vile  uji,  maziwa, ugali, biskuti , keki n.k 

UMUHIMU WA SOYA:

1. Soya ina viini lishe aina ya protini kwa wingi kuliko jamii zote za mikunde na hata  baadhi  ya  protini  zinazotokana  

na wanyama.  

2. Soya ni chanzo rahisi na chenye gharama  nafuu cha protini  inaweza kulimwa maeneo mengi hapa nchini. 

3. Kwa kuwa soya ina kiasi kikubwa cha protini kupunguza kasi ya  mashambulizi ya vijidudu vya maradhi mbalimbali    ikiwa    ni    pamoja na magonjwa ya kansa, moyo, na  kuwaongezea  nguvu  wagonjwa  hasa  wa UKIMWI;  

4. Soya ni zao muhimu kwa watu wa kipato cha chini katika  kuondoa utapiamlo.   

5. Kutokana na uwingi wa protini, matumizi ya soya kwa watoto  yanasaidia viungo kukua kwa haraka;  

6. Soya hurutubisha udongo.  

7. Soya huongeza kipato na ni zao linaloweza  kuchangia  katika  kuondoa umaskini.  

8. Utafiti unaonyesha kuwa mafuta ya soya yanaweza kutumika kwa kuendeshea mitambo yaani  

bio-fuel na bio-diesel.

(Kwa kujua zaidi kuhusu kilmo cha zao la Soya wasiliana na mtaalamu wa Davidi Chacha kwa namba ya simu 0753-953260)


No comments

Powered by Blogger.