TARI KUSHIRIKIANA NA WAKULIMA KWENYE UTAFITI WA MBEGU
................................
Na Grace Hamisi, Mtwara
TAASISI ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) inatarajia kuanza kushirikiana
na wakulima kufanya utafiti wa mbegu bora.
Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa TARI, Dkt. Thomas Bwana wakati wa ziara
yake ya kikazi aliyoifanyi hivi karibuni
katika kituo cha utafiti wa kilimo (TARI) Naliendele ambapo pia alipata
fursa ya kutembelea sehemu za uzalishaji wa miche ya mikorosho na michikichi
pamoja na kiwanda cha kubangua korosho kilichopo kituoni hapo.
Dkt. Bwana alisema kuwa kwa sasa TARI imejipanga kuwashirikisha wakulima
katika utafiti wa uzalishaji wa mbegu ili kusaidia na wao kujitengenezea mbegu zilizo bora.
"Katika siku zijazo tunataka mkulima wa korosho awe na misimu miwili
wa korosho, karanga na msimu wa bibo kwani siku hizi bibo linaonekana ni kitu
cha kutupwa kumbe kuna bidhaa ambazo zinapatikana kama mvinyo (wine), Ethanol
inayotokana na bibo pamoja na juisi ya bibo hivyo tunahakikisha kuwa tunapata
bidhaa zote katika ngazi ya kibiashara," alisema Bwana.
Aidha Dkt Thomas meongeza kuwa (TARI) Naliendele
imefanya vizuri kwenye utafiti wa korosho kwa upande wa magonjwa ya ubwiri unga
huku aina nane (8) za mbegu za korosho zilizofanyiwa utafiti na kubainika
kuwa na uhimilivu mkubwa wa magonjwa.
Hata hivyo Dkt Bwana alisema kwa sasa wanataka
kuwapa wakulima fursa ya kujaribu mazao tofauti na waliyoyazoea kama migomba na
michikichi kutokana na mimea hiyo kuwa na uhitaji mkubwa katika
uazalishaji wa mafuta ambayo ni sehemu ya mkakati wa kitaifa katika
uzalishaji wa mafuta ili kuachana na uagizaji kutoka nje ya nchi.



No comments