Header Ads

TARI YAONESHA TEKNOLOJIA YA KILIMO BORA CHA NDIZI AINA YA FHIA 23, TARIBAN MAONESHO YA SABASABA 2024

FHIA 23 na TARIBAN 4 ni Miche za Migomba iliyofanyiwa Utafiti na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) ambayo Mkulima na wadau wa Kilimo na Biashara waofika Banda la TARI katika maonesho ya biashara Viwanja vya Julius Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam walipata fursa ya kujifunza namna ya kunufaika na matokeo ya Utafiti huo.

SIFA ZA MICHE YA FHIA

1. Huzaa Mikungu mikubwa yenye chane nyingi hivyo inafaa kwa Biashara.

2. Mavuno yake ni Tani 60-80 kwa mwaka kwa hekta.

3. Miezi sita baada ya kupandwa Inatoa machipukizi mengi 7-9 Kwa mche mmoja ambayo ni fursa ya kuongeza kipato (biashara).

4. Inaradha nzuri inapopikwa, pia inafaa kwa kuivisha.

5. Kukomaa kwake ni mwaka Mmoja na miezi mitano hadi mwaka Mmoja na miezi nane toka kupandwa kwake.

6. Inastahimili mashambulizi ya magonjwa mbalimbali katika zao la mgomba kama vile; ugonjwa wa mnyauko fusari, madoa meusi, Bungua wa Migomba na Minyoo fundo.

No comments

Powered by Blogger.