Header Ads

TARI NALIENDELE YAFUNDISHA TEKNOLOJIA YA UVUNAJI WA ZAO LA UFUTA

Mratibu wa programu ya zao la ufuta kitaifa wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI)  Naliendele  Joseph Mzunda akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoa elimu ya namna bora ya uvunaji wa ufuta kwa wakulima .

......................................

Na Mwandishi Wetu, Mtwara

 

WAKULIMA na wadau wa zao la ufuta nchini wametakiwa kuzingatia ubora kwa kuanzia katika hatua za awali za kulima, uvunaji na utunzaji wa zao hilo ili kuendana na mahitaji ya soko linavyotaka.

 Hayo yalisemwa na mratibu wa programu ya utafiti wa ufuta kitaifa na mtafiti wa zao la ufuta kutoka TARI Naliendele Joseph Mzunda wakati akitoa elimu ya namna bora ya kulima na kuvuna zao hilo kwa baadhi ya wakulima ambapo alisema kuwa wadau wa zao la ufuta lazima waangalie kuwa linapofika mikononi mwao lipo katika hali ya usafi ili kusitokee  lawama kutoka kwa wanunuzi.

Aidha Bw  Mzunda alisema kuwa wanunuzi wa ufuta wamekuwa na vigezo maalumu vinavyowafanya kununua ikiwepo ubora,rangi na Ladha yake huku akielezea  upekee unaopatikana kwenye ufuta unaozalishwa nchini ukilinganisha na nchi nyingine.

Mtafiti wa zao la ufuta kutoka TARI Naliendele akitoa maelezo kwa wakulima namna bora ya kuvuna na kukausha ufuta

Hata hivyo Bw Mzunda amewataka wakulima kutunza kiasi cha fedha kwa ajili ya kununua mbegu zilizokuwa bora na kwa ajili ya pembejeo na viuatilifu ili iwasaidie kutumia katika msimu unaofuata  wa kilimo cha ufuta.

Fatma Athumani na Aisha Wilson wakulima wa zao la ufuta kutoka Kata ya Naliendele wamesema kupitia elimu waliyoipata kutoka TARI itawasaidia katika kuandaa mashamba na namna bora ya kuvuna zao hilo tofauti na hapo awali walivyokuwa wakilima.Wakulima wa zao la ufuta wakionesha njia bora ya kuvuna zao hilo na kuutunza.

 

No comments

Powered by Blogger.