AGRICOM AFRIKA YAJIVUNIA MAFANIKIO USAMBAZAJI MASHINE ZA KILIMO KWA WAKULIMA
Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
KAMPUNI inayomilikiwa na mwanamke wa Kitanzania ya Agricom Afrika Limited iliyoanzishwa mwaka 2009 inajivunia mafanikio katika usambazi wa mashine za kilimo ambapo kwa mwaka 2019 jumla ya matrekta 400 wamepewa wakulima.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na waandishi wa habari Machi 14,2025 Ofisini kwake jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni hiyo, Elias Leasa, alisema mbali ya matrekta hayo kampuni hiyo ilikabidhi Wizara ya Kilimo matrekta 100.
Leasa alisema mafanikio ambayo kampuni hiyo imeyapata yametokana na juhudi kubwa zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuinua kilimo ambacho kinatoa ajira nyingi kwa Watanzania hususani vijana.
“Kampuni yetu ni ya kwanza kwa usambazaji wa mashine bora za kilimo kama vile za umwagiliaji, matrekta na nyingine nyingi ambazo zimeongeza uzalishaji wa mazao nchini, “ alisema Leasa.
Leasa alitumia nafasi hiyo kuiomba Serikali kuendelea kuwekeza kwenye kilimo ili kutengeneza ajira nyingi jambo litakalosaidia kutoa ajira na kuwepo kwa uhakika wa chakula nchini.
Aidha, Leasa alisema katika zana za kilimo Serikali imeondoa kodi kama za uingizaji wa matrekta lakini kwenye matrela yanayokokotwa na matrekta haijaondolewa hivyo anaomba na kwenye eneo hilo pia iondolewe.
Leasa alisema hakuna mafanikio yasiyokuwa na changamoto akitolea mfano mafuriko yaliyowakumba baadhi ya wakulima na kusababisha kukosa fedha kwa ajili ya kununulia vitendea kazi.
Alisema mwaka 2024 wakulima wengi waliuza mazao kwa bei ya chini tofauti na matarajio hali ambayo ilisababisha kuuza mazao mazao yao kwa bei ya hasara hivyo ameiomba Serikali iangalie namna yakuwasaidia wakulima hao ili waweze kuuza mazao yao kwa bei ya uhakika hatua itakayowasaidia wawe na uwezo wa kununua zana zitakazo warahisishia katika ufanyaji wa kilimo.
“ Mkulima anapokutana na changamoto huwa anashindwa kununua vitendea kazi kama trekta na badala yake ukimbilia kununua pawatila ambayo bei yake ni ya chini,” alisema Leasa.
Leasa alitaja aina ya matrekta wanayo yasambaza kuwa ni Kubota EK 4, Swaraj 975 na Swaraj 744 FE ambayo ni imara na yenye na kuwa yanatumika maeneo mengi nchini na bei yake nafuu.
Alisema kampuni hiyo imekuwa na mafanikio kwa mtindo wa kikanda ambako wana mawakala wao na baadhi ya mikoa wamefungua ofisi ambazo zina simamia uzambazaji wa bidhaa zao na kufungua karakana za utengenezaji wa mashine na matrekta ili kumpunguzia mkulima gharama za kwenda kutengeneza zana hizo pale zinapokuwa na changamoto za kiufundi.
Alisema wanakanda tano ambazo amezitaja kuwa ni Kanda ya Mashariki na Pwani (Dar es Salaam,Morogoro,Tanga,Lindi, Mtwara) Kanda ya Kati Dodoma,Singida, Manyara, Arusha,Kilimanjaro), Kanda ya Ziwa (Mwanza, Mara,Simiyu, Shinyanga, Kagera, Geita),Kanda ya Magharibi (Rukwa, Kigoma, Katavi),Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (Mbeya,Songwe,Iringa,Ruvuma)
Akizungumzia ushiriki wao katika Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima Nanenane alisema wao ni wadau wakubwa wa maonesho hayo ambapo ameeleza kuwa kwa mwaka huu 2025 watakuja kivingine kwani wataingiza bidhaa za ufugaji kwa kuzingatia kuwa kilimo na ufugaji ni kama Ardhi na Maji.
Alisema katika maonesho hayo watakuwa na bidhaa za kisasa kama vile za kukamulia maziwa na kupakia ambazo zitamsaidia mfugaji kufanya kazi za ke kwa ubora na usalama na mashine za kubangulia karanga.
Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Agricom Afrika Limited, Elias Leasa, akisisitiza jambo wakati wa mahojiano hayo.
Mkuu wa Uendeshaji wa Kampuni ya Agricom Afrika Limited, Elias Leasa, akionesha Trekta aina ya Waraj 963 FE ambayo ni bora kwa matumizi.
Muonekano wa eneo la kuegesha mashine na matrekta yanayosambazwa na kampuni hiyo. ' Hakika ni Tabasamu Shambani, Tabasamu Sokoni'


.jpg)



No comments