MNYETI ATEMBELEA MRADI WA SAMAKI KWA NJIA YA VIZIMBA NYAMAGANA MWANZA
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Alexander Mnyeti (Mb) ametembelea mradi wa Ufugaji wa samaki Kwa njia ya Vizimba uliopo Mtaa wa Kisoko, kata ya Luchelele Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza, ambapo amepata fursa ya kushuhudia namna Wanufaika wa Mradi huo wanavyojishughulisha na shughuli za uzalishaji wa Kila siku.
Katika ziara hiyo, Mhe Mnyeti alipata fursa ya kuwaeleza Vijana hao Mikakati ya Serikali katika uwekezaji huo ikiwemo ugawaji wa Vizimba kwa awamu ya pili ambao utaenda sambamba na ugawaji wa Boti za Kisasa, kama sehemu ya kuwainua Wananchi kiuchumi.



No comments