Header Ads

KAMPUNI YA MZURI AFRIKA YATAMBULISHA MASHINE ZA KISASA ZA KILIMO, HIYO NI FURSA KWA WAKULIMA

Mashine moja inalima hekari 10 kwa saa moja

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mzuri Afrika Shaban Mgonja, akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuleta mashine za Teknolojia  ya Kisasa za kilimo jijini Dar es Salaam.

.........................................

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya Mzuri World imeleta mapinduzi kwa kuzindua mashine za kisasa za kulimia, kupanda, na kunyunyizia dawa shambani

Kaampuni hiyo ambayo inazalisha mbolea za kimiminika tayari imesajili aina 11 za mbolea hapa nchini.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampumi hiyo, Shaban Mgonja, akizungumza na waandishi wa habari Machi 7, 2025 alisema uletaji wa mashie hizo kunalenga kuboresha kilimo cha Tanzania kwa kutumia teknolojia za kisasa ambazo zinapunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija kwa wakulima sambasamba na kulinda ardhi.

"Mimi ni Mtanzania, na kwa kutambua kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu, nimeona ni muhimu kuleta teknolojia itakayosaidia wakulima kuongeza uzalishaji wao kwa ufanisi mkubwa," alisema Mgonja.

Alisema Mashine ya Mzuri si ya kawaida, kwani inachanganya hatua tatu muhimu za kilimo: kulima, kupanda mbegu, na kuweka mbolea kwa wakati mmoja.

Amesema Teknolojia hiyo imeenea katika nchi 50 duniani, na sasa Tanzania ni moja ya nchi zinazofaidika na utumiaji wa teknolojia.

Alisema mashine hiyo inapatikana katika ukubwa tofauti, ikiwa na urefu wa wa mita 3 na inalima heka 6 kwa saa moja, Mashine ya mita 4 inalima heka 10 kwa saa moja pamoja na Mashine ya mita 6 inalima heka 15 kwa saa moja.

Mgonja alisema mashine za Mzuri zinapunguza muda wa kazi, gharama za uendeshaji, na kuhakikisha kilimo kinakuwa cha kisasa na chenye faida

" Ili kuhakikisha wakulima wanaelewa vizuri manufaa ya mashine hii, kampuni yetu ya Mzuri World imeandaa shamba maalumu lenye ukubwa wa heka 300 lililopo Vigwaza, Kibaha – mkoani Pwani, ambako wakulima wanaweza kuona kwa vitendo jinsi teknolojia hiiyo  inavyofanya kazi," alisema Mgonja.

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Mzuri World, Marek Rozniak, amesema kuwa lengo la kampuni hiyo si kuuza mashine tu, bali pia kusaidia wakulima kutumia teknolojia mpya ili kuokoa muda, mbegu, na mbolea huku wakipata mavuno mara dufu.

"Teknolojia ya Mzuri inasaidia wakulima kutumia raslimali zao kwa ufanisi mkubwa. Kwa kutumia mashine hizi, mkulima anaweza kupunguza gharama za uzalishaji huku akiongeza mavuno yake kwa kiwango kikubwa," alisema Rozniak.

Amesema kwa maendeleo hayo kwa wakulima wa Tanzania sasa wana fursa ya kubadili mfumo wa kilimo kutoka wa jadi kwenda wa kisasa, jambo ambalo litasaidia kuongeza uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara kwa tija zaidi.

Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Mzuri World, Marek Rozniak, akizungumzia umuhimu wa matumizi ya mashine hiyo.
Viongozi wa kampuni hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wao.
Picha ya pamoja wakati wa kutambulisha mashine hiyo.
 

No comments

Powered by Blogger.