SUMU KUVU ILIVYOATHIRI WATOTO BABATI MANYARA
Imeelezwa kuwa baadhi ya watoto wa kuanzia umri wa miezi 6- 24 wilayani Babati mkoani Manyara wameathiriwa na changamoto ya sumu kuvu kutokana na jamii kutokuwa na uelewa wa kuhifadhi mazao katika sehemu salama.
Na Mwandishi Wetu, Babati
Kufuatia utafiti uliofanyika wilayani Babati mkoani Manyara
asilimia 70 ya watoto wamekutwa wameathiriwa na sumu kuvu itokanayo na vyakula
wanavyovitumia, ambapo wazazi na walezi mkoani Manyara wametakiwa kuandaa
vyakula bora ili kuwalinda watoto.
Hayo yameelezwa leo na Naeliwa Mshanga ambaye ni mwanafunzi wa
uzamivu NMAIST katika semina iliyoandaliwa na shirika la Oikos East Africa na
kuwakutanisha wadau mbalimbali wakiwemo wanawake wanaonyonyesha,
maafisa lishe, maafisa kilimo, mganga mkuu, wawakilishi kutoka Imperial uUniversity,
Leeds University na Nelson Mandela University.
Amesema kwa utafiti ambao ulifanyika mwaka 2022 umebaini
kuwa hali ya sumu kuvu katika wilaya ya Babati ni asilimia 70 na kupelekea
kuwepo kwa udumavu ukiwa na asilimia 32, kilo pungufu asilimia 20 na ukondefu
asilimia 4.
Kufuatia tafiti hizo afisa kilimo mkoa wa Manyara Paulo Eugene,
amewataka wakulima kukausha na kuhifadhi vizuri mazao Ili kudhibiti sumu
kuvu kuingia kwenye mazao.
Naye mwakilishi wa mganga Mkuu wa Wilaya ya Babati Jacobo Mwanamtwa
amewataka wazazi na walezi kupanga utaratibu wa vyakula kulingana na umri wa
watoto ambapo amesema wanaendela kutoa elimu hiyo Kila kijijji juu ya umuhimu
wa lishe Bora Kwa watoto.
Aidha , Dr Monica Pirani ni mtafiti mkuu wa chuo kikuu Cha
Imperial university London amesema hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kudhibiti
tatizo Hilo ni pamoja na kuongeza elimu ya lishe Ili kuhamasisha jamii
kupambana na utapiamlo pamoja na kuimarisha huduma za afya Ili kufikia vijiji
vya mbali zaidi.
Nao baadhi ya wanawake wanaonyonyesha ambao wameshiriki katika
semina hiyo, wamewashukuru waandaaji wa semina hiyo kwani elimu ambayo
wameipata imewasaidia kufahamu namna ya kuepuka sumu kuvu katika vyakula
wanavyoviandaa.



No comments