Header Ads

MAYAI YA DR. FLAVE YENYE KIINI CHA RANGI YA MANJANO YANAPATIKANA MWAKA MZIMA

Muonekano wa mayai ambayo yapo tayari sokoni
Muonekano wa kiini cha manjano kwenye mayai

.................................................. 

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam 

UFUGAJI wa kuku wa mayai wenye viwango vya juu umekuwa ukichochea lishe bora kwa jamii kutokana na ulaji wa mayai hayo. 

Jijini Dar es Salaam mayai ya Dr. Flave yamekuwa ni kimbilio la watu wengi kutokana na ubora wake. 

Meneja Masoko wa Kampuni ya Dr. Flave inayo zalisha mayai hayo Bi. Linda Byaba anasema kutokana na mahitaji makubwa ya mayai hayo wamelazimika kuongeza uzalishaji ili kukidhi mahitaji ya wateja wao. 

“Hatua tuliyoichukua ya kufuga kuku kwa wingi imeongeza idadi kubwa ya mayai kununuliwa, kwetu ni mafanikio makubwa,” alisema Byaba. 

Alisema wamekuwa wakizingatia ufugaji bora na kuwa kuku wao wanatumia chakula cha asili tofauti na ule ufugaji unaotumia vyakula vya viwandani hivyo kutokana na matumizi hayo ya vyakula vya asili kuku wanao wafuga wamekuwa wakitaga mayai yaliyo bora. 

“Mayai yetu yana sehemu nyeupe pamoja na kiini cha rangi ya manjano ambayo vimejaa virutubisho vyenye protini, vitamini na madini huku kiini cha manjano kikiwa kina aina nyingi za vitamini na ile sehemu nyeupe ya yai ikiwa na kiwango kikubwa cha protini. 

Byaba anasema kutokana na hatua hiyo ya kuongeza ufugaji wana mayai ya kutosha ambayo yapo kwa msimu mzima wa mwaka hivyo kwa mtu atakaye hitaji hata zaidi ya trei 100 atapata pasipo mashaka yoyote.  

Alisema mteja au mtu yeyote anayehitaji mayai hayo anaweza kutoa oda kupitia Instagram yao @dr.flave2 au @dr.flave au WhatsApp na simu ya kawaida namba 0677303000 

No comments

Powered by Blogger.