Header Ads

SOSEJI ZA DR. FLAVE: ZAWA GUMZO, ZAWALIZA WATOTO, ZINAPATIKANA MIKOCHENI B JIJINI DAR ES SALAAM



Muonekano wa Soseji za Dr. Flave

............................................. 

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam

SOSEJI ni chakula kilichotengenezwa kwa nyama iliyosagwa au kukatwa kwa vipande vidogo, kuchanganywa na chumvi na viungo halafu kujazwa katika sehemu za utumbo au mirija ya plastiki. Kwa aina mbalimbali za soseji viwango vya nafaka au mkate vinaweza kuongezwa katika mchanganyiko.

Jina soseji limeingia katika Kiswahili kutoka Kiingereza "sausage"; asili yake ni Kilatini "salsica" yenye maana ya "iliyotolewa chumvi".

Vipande virefu vinavyotokea baada ya kujaza hutenganishwa kwa kufunga sehemu kwa kamba au kuviringisha vipande vinavyoweza kukatwa baada ya kupika.

Soseji nyingi hupikwa baada ya kutengenezwa. Aina nyingine zinawekwa katika moshi juu ya moto zikiiva humo kwa muda wa siku au wiki kadhaa. Aina kadhaa hukauka tu hewani.

Soseji za kupikwa zinaweza kufungwa katika makopo maalumu au glasi ambako zinaweza kudumu kwa muda mrefu.

Halikadharika huwekwa kwenye mifuko au vifungashio maalumu na hutunzwa kwa kuwekwa kwenye majokofu (Friji) kwa zile ambazo ni fresh ila zingine huhifadhiwa kwenye vifungashio hivyo malumu na kutunzwa kwenye mazingira ya baridi la kawaida.

Siku hizi soseji hutengenezwa mara nyingi kiwandani kwa kutumia mashine zinazosaga nyama nyingi na kutengeneza soseji mfululizo.

Soseji zimetengenezwa tangu kale. Kwa upande moja ni njia ya kutunza nyama kwa muda kabla ya matumizi kwa kuongeza chumvi inayoozuia bakteria na kuziweka katika moshi inayozuia wadudu kutaga mayai kwenye soseji. Mbinu hiyo ni vigumu katika mazingira ya joto pasipo jokofu.

Soseji zinaweza kuliwa peke yake, pamoja na mkate baridi, zinaweza kupikwa pamoja na mboga ya majani..

Ziko aina zinazofaa kuliwa bila kupashwa moto.

Nchi nyingi na hata mikoa kadhaa huwa na soseji za pekee zinazotofautiana katika ladha na mwonekano.

Lengo la kuanza na utangulizi huu ni kutaka kueleza kwa kifupi  jinsi ya kitoweo hicho kinavyo tengenezwa na leo napenda kuzungumzia Soseji za Dr. Flave zinazotengenezwa na Kampuni ya  Dr. Flave kwa kushirikiana na Kilimo Joint yenye ofisi zake  Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.

Soseji za Dr. Fave zimejizolea umaarufu mkubwa na kutokewa kupendwa na wakazi wa Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi  kutokana na kuwa na ladha nzuri na kuzifanya soko lake kuwa kubwa.

Hali hiyo inatokana na jinsi zinavyotengenezwa na kuandaliwa na wataalamu wa mapishi ambao ni wabobezi wa kimataifa na kuzifanya zinunuliwe na watu kutoka ndani ya nchi na mataifa mbalimbali na bei zake ni nafuu.

Meneja Masoko wa kampuni hiyo Linda Byaba anasema  kampuni yao inajishughulisha na ufugaji wa kuku, kuku wa nyama na kuku wa mayai na pia kutoa ushauri wa ufugaji pamoja na uzalishaji wa soseji za ng’ombe maarufu kama soseji / mtura.

  “Soseji zetu zimetokea kupendwa hasa na watoto ambao wazazi wao wamekuwa wakipongeza kutokana na kutengenezwa kwa viwango vya juu na kuwa na ladha nzuri ambao mara kwa mara wamekuwa wakitoa oda kwa ajili ya watoto wao ambao wamekuwa wakizililia kutokana na utamu wake,” alisema Byaba.

Alisema kampuni hiyo inaziandaa soseji hizo ambapo wateja wao wanakwenda kuzipika kulingana na mahitaji ya mapishi yao binafsi majumbani kwao na mahotelini.

Akizungumzia upatikanaji wa soseji hizo, Byaba alisema wanapokea oda kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini ikiwemo  Mwanza, Iringa, Mbeya na kuwa bidhaa hiyo inawafikia kwa wakati mara baada ya kukamilisha malipo.

Meneja masoko huyo anasema wanamzigo wa kutosha wa Soseji za Dr. Flave  na kuwa sasa zinapatikana kuanzia nusu kilo na kilo na kuwa oda za mikoani wanazipokea siku mbili kabla.

Alisema mteja au mtu yeyote anayehitaji soseji hizo anaweza kuwasiliana na Dr. Flave na kutoa oda kupitia Instagram yao @dr.flave2 au @dr.flave au WhatsApp au kwa namba ya simu ya kawaida ambayo ni 0677303000  

 Muonekano wa Soseji hizo za Dr. Flave

Soseji za Dr. Flave
 

No comments

Powered by Blogger.