Header Ads

MIPANGO BORA YA MATUMIZI YA ARDHI YASISITIZWA KUONDOKANA NA MIGORORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) amefanya ziara ya kikazi Mkoani Tanga katika wilaya ya Handeni ambapo pia amepata fursa ya kuongelea suala la mgogoro wa wakulima na wafugaji.  

Ziara hiyo imeanza tarehe 13 Februari 2026 ambapo Waziri Mkuu Nchemba alipata wasaa wa kusikiliza migogoro ya wakulima na wafugaji ambapo mkulima Bw. Omari Athumani, mkazi wa Jimbo la Mkata Mashariki alieleza kero za wafugaji kulisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima.  

Akizungumzia Sekta ya Kilimo kuhusu hoja iliyotolewa na mkulima huyo, Waziri wa Kilimo Mhe. Daniel Chongolo (Mb) amesema “mifugo ni sehemu ya wakulima katika mazingira ya kazi na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.  Nimeongea na Waziri Mwenzangu Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Kakurwa ili kwa kushirikiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kupima na kutenga maeneo rasmi kwa ajili ya wakulima na wafugaji katika kuondokana na kero zao,” Amesema Waziri Chongolo. 

“Wakulima ni watanzania na wafugaji ni watanzania, na wote kama watanzania tunaruhusiwa kuishi kokote nchini.  Kitu muhimu na cha msingi tufuate taratibu.  Idadi ya watu inaongezeka lakini ardhi inapungua.  Tufuate taratibu na kuepusha migogoro yoyote. Kosa la mfugaji mmoja siyo la wafugaji wote; tusitengeneze ufa,” amesisitiza Waziri Mkuu Nchemba. 

Ameelekeza anayefanya kosa kama mfugaji hatua za kisheria zichukuliwe kwa aliyehusika na sikuhukumu jamii yote ya wafugaji.  “Ukitokea umeteleza usifanye kiburi.  Hakuna ubabe na jeuri katika kuvunja sheria.  Kila mmoja afanye shughuli ya maendeleo kwa kuzingatia sheria, katiba na undugu,” amesema Waziri Mkuu Nchemba. 

No comments

Powered by Blogger.