WIZARA YA KILIMO YAANDAA MAFUNZO YA USIMAMIZI WA MIRADI NA MIKATABA
Wizara ya Kilimo imeandaa mafunzo kwa kushirikiana na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) yenye lengo la kuwajengea uwezo Wahandisi wa Wizara na Taasisi zake katika masuala ya usimamizi bora wa miradi na mikataba kwa kuzingatia misingi ya uwajibikaji, ufanisi na thamani ya fedha.
Katibu Mkuu Mweli amesisitiza washiriki kujifunza kwa bidii na kutumia ipasavyo maarifa watakayoyapata ili kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Amesema mafunzo hayo ni sehemu ya mkakati wa Wizara kuimarisha rasilimali watu na kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa viwango vinavyokidhi matarajio ya Serikali na wananchi.
Ameongeza kuwa usimamizi madhubuti wa miradi na mikataba ni nguzo muhimu katika kufanikisha malengo ya Sekta ya Kilimo, hususan katika kipindi ambacho Serikali inaendelea kuwekeza katika kuboresha miundombinu na zana za kisasa za kilimo.



No comments