ASA YAAGIZWA KUJENGA GHALA NA KIWANDA NZEGA
Amesema hayo wakati wa ziara yake tarehe 18-19 Mei 2024 Wilaya ya Nzega
ambapo amekagua maendeleo ya uzalishaji wa mbegu kwenye shamba hilo ambalo
limeshawekewa miundombinu ya umwagiliaji ili liweze kuzalisha mbegu bila
kutegemea mvua.
Naibu Waziri Silinde amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Samia Suluhu Hassan alikuwa na maono ya kuiwezesha nchi kuzalisha mbegu za
mazao na ili kuhakikisha malengo ya Mhe. Rais yanatimia lazima lijengwe ghala
madhubuti la kuhifadhia mbegu na kukamilika ifikapo mwezi Oktoba 2024 ambapo
litahakikishia wakulima uhakika wa mbegu kama alivyokusudia Mhe. Rais.
Aidha, Mhe. Silinde ameagiza kuanza kwa mchakato wa upatikanaji wa kiwanda
cha kusindika mbegu ndani ya shamba hilo ili kuepuka gharama za kusafirisha
mbegu hizo kwenda kiwandani mjini Morogoro na baadae kurudishwa tena kwa
wakulima.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mbegu za Kilimo (ASA), Dkt.
Sophia Kashenge amesema anatambua na kupongeza ushirikiano wa viongozi wa
Wizara ya Kilimo kwa ASA unaopelekea kuimarika kwa shughuli za wakala huo.
Shamba la ASA la Kilimi lina ukubwa wa hekta 11000 ambapo eneo lililotumika
hadi sasa ni hekta 802.5. Aidha, kwa
sasa shamba hilo limezalisha mbegu za mahindi hekta 50 za mtama, hekta 40 za
alizeti, hekta 10 za choroko na hekta 250 za mahindi.



No comments