Header Ads

UZALISHAJI WA MAWESE KUONGEZEKA NCHINI

Uzalishaji wa mafuta ya mawese nchini unatarajiwa kuongezeka baada ya mipango iliyoainishwa ya kuifanya nchi kujitegemea katika upatikanaji wa mafuta ya kupikia na kuuza nje ya nchi kufanyika kwa kupitia ushirikiano kati ya Tanzania na Indonesia.

Msukumo mpya wa uzalishaji utaelekezwa katika mkoa wa Kigoma, ukanda wa kilimo cha jadi cha michikichi na baadaye mikoa mingine ikiwamo Mbeya.

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (Tari) kupitia vituo vyake vya Tumbi na Kihinga katika mikoa ya Tabora na Kigoma watajumuishwa katika mpango wa mafuta ya mawese. 

Chanzo:- Dr.Dwi Asmono, Mkurugenzi wa Kampuni ya Biashara ya Kilimo ya Indonesia iitwayo Sampoerna Agro

Mkoa wa Kigoma unazalisha 80% ya mafuta ya mawese kila mwaka.

Makampuni ya Indonesia yataungana na Tari na taasisi washirika katika kuanzisha aina za michikichi zinazozaa kwa wingi kupitia utumiaji wa mbinu sahihi za kilimo.

Hivi sasa, inakadiriwa kuwa 80% ya mafuta ya kupikia yanayotumiwa nchini Tanzania yanatokana na mafuta ya alizeti, hivyo ongezeko la mafuta ya mawese itaifanya Tanzania kuwa na mafuta toshelevu kwa matumizi ya ndani na kuuza nje ya nchi.

No comments

Powered by Blogger.