CHONGOLO AKABIDHIWA OFISI NA KUSISITIZA KUKUZA SEKTA YA KILIMO NCHINI
Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Godfrey Chongolo akipeana mkono na Waziri wa Kilimo aliyemaliza muda wake Mhe. Hussein Bashe katika hafla ya kukabidhiana ofisi.
..........................................
Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Waziri wa Kilimo, Mhe. Daniel Godfrey Chongolo (Mb) ameieleza Menejimenti na Watumishi wa Wizara ya Kilimo kuwa kazi na malengo yaliyopangwa yatafikiwa kwa kuendeleza pale Mbunge wa Nzega Mjini, Mhe. Hussein Bashe alipoishia ili kukuza na kuleta tija kwenye Sekta ya Kilimo nchini.
Chongolo amempongeza Waziri wa Kilimo aliyemaliza muda wake Hussein Bashe, Menejimenti na Watumishi wa wizara hiyo kwa ujumla kwa kuwa mstari wa mbele katika kubuni miradi mbalimbali ambayo imekuwa ikileta tija na manufaa kwa wakulima na Taifa.
Mhe. Waziri Chongolo amesema hayo wakati akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano ya ofisi na Mhe. Hussein Bashe (Mbunge wa Nzega Mjini), Novemba 18, 2025, katika Ukumbi wa Wizara, jijini Dodoma.
Halfla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde (Mb), Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Gerald Mweli na Naibu Katibu Mkuu anayesimamia Umwagiliaji na Zana za Kilimo, Mhe. Athumani Kilundumya; wakiwemo Wakurugenzi Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Kilimo zilizopo jijini Dodoma.
Kupitia hafla hiyo, Mhe. Bashe amempongeza Waziri Chongolo kwa kuteuliwa kuwa Waziri wa Kilimo na kumhakikishia ushirikiano wakati wowote katika kufanikisha maono makubwa ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sekta ya Kilimo.
Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo akifurahi na Mhe. Hussein Bashe na Naibu Waziri wa Kilimo, Mhe. David Silinde katika hafla ya makabidhiano ya ofisi.
Waziri wa Kilimo Daniel Chongolo akifurahi na Mhe. Hussein Bashe wakiwa wamekumbatiana kwenye hafla hiyo,
Mkutano ukifanyika wakati wa makabidhiano hayo.
Picha ya pamoja



No comments